coutinho na liverpool 2017
| philipe coutinho |
Twaweza sema kuwa kwa kila timu basi kunakuwa na kiongozi, sio lazima awe nahodha lakini yaipasa kila timu kuwa na mchezaji ambaye uchezaji wake utaweza kuibeba timu nzima kwa msimu husika. Kwa upande wa majogoo wa jiji la anfield liverpool FC, mchezaji mnyumbulifu mzaliwa wa Brazil COUTINHO ameonesha kuwa ndiye mchezaji muhimu sana chini ya kocha wa kijerumani Jurgen Kloop.
Tangu msimu uanze, imekuwa ni suala wazi kabisa kuwa ili liverpool ishinde mechi basi haina budi kwa Coutinho kuwa katika kiwango mujarabu. Uwezo wake wa kutengeneza nafasi kwa ajili ya wachezaji wengine umekuwa wa hali ya juu, uwezo wake wa ufungaji magoli pia umekuwa katika kiwango bora, amekuwa ni mchezaji pekee katika kikosi cha liverpool ambaye amepewa uwezo wa kucheza takribani kila sehemu ya uwanja, akipewa uhuru wa kufanya lolote uwanjani na kocha wake kloop.
Mzaliwa wa Brazil mwaka 1992, Coutinho kama ilivyo tamaduni nchini humo amekuwa akipenda mchezo wa mpira wa miguu tangu akiwa mdogo.
Umuhimu wake katika kikosi cha liverpool msimu wa 2016/2017 umeonekana wazi pale alipopata majeraha katika mchezo dhidi ya sunderland 26 novemba 2016. Kuumia kwake kumekuwa pigo kubwa sana ukizingatia alikuwa tiyari katika hali nzuri kiuchezaji akifunga magoli matano na kusaidia kutengeneza mengine matano akisaidia timu yake kukaa kileleni mwa ligi. Baada ya kuumia liverpool imeachia usukani wa msimamo wa ligi na mpaka sasa iko nafasi ya nne, mbio zake za kulisaka kombe ambalo hawajalipata miongo zaidi ya miwili sasa zinaaza kufifia.
Ni wazi kuwa kuumia kwa Coutinho ndio sababu kubwa ya liverpool kushuka kiwango kama timu maana alikuwa anawafanya wachezaji wamzungukao kucheza vema zaidi. Hivyo twaweza pia kusema kuwa kupona kwake ni neema sana kwa liverpool na bila shaka itakuwa timu kabambe kukiwa na Coutinho katika kikosi.
wengine walienda mbali na kusema kuwa katika kipindi kile hajapata majeraha ndiye aliyekuwa mchezaji bora wa epl huku vilabu vikubwa duniani kama barcelona vikiiota saini yake....
ReplyDelete